Wednesday, June 26, 2024

Check Hapa Kinachoendelea Kwenye Lipa Za VODA


Narudi tena WAKALA Usipochukua Tahadhari 

Mbili Mhimu (Nimezitaja mwishoni)

Basi Utajikuta Bila Kutarajiwa UMEFIRISIWA

Mtaji wako wote Ndani Ya Siku Moja..


NA..

Kabla Sijafichua Tafadhari mbili Za kuchua


Kwanza...


 Angalia  Picha3  

Zinayofuata Chini 



1.

Huyu WAKALA Tayari Lipa Yake
Wameifunga (FROZEN)

kama Unavyoona



Checki MSALA 
Mwingine




Huyu Yeye wamempandishia Makato 



Checki Mwingine tena




Huyu yeye wamempiga

Pini Ukomo Wa kutoa 
Mwisho
Sh 4999SH..kwa siku..

HIVYO 

ILI YASIKUPATE...

EPUKA KUFANYA YAFUATAYO:

1.Usithubutu Kamwe Kutolea Lipa
Yenye Majina Sawa na Till yako ya VODA 

2.Acha Kabisa Kuhamisha Flot Ya Lipa kwenye Lipa Zingine Kisha unazitolea Kwenye Till Ako Ya VODA 


Ukizingatia Hayo Mawili 

LIPA yako itakuwa Salama


PIA..


Endelea Kugundua Zaidi SIRI Zingine Kuhusu 

Lipa na mitandao ya simu Kwenye POST zinazofuata Chini...










Saturday, June 22, 2024

Sababu Tano Za Kukatwa Kamisheni Na Jinsi Ya  Kuziepuka


 JE VODA wanakukataga Kamisheni...?

.

Ukijua Hii SIRI mwiko kukatwa tena..

.

Najua unahasira sana..

.

Juu ya VODA kukukata Commission..

 

Kwa Sababu kila mwezi..

.

 Unajitadi Kweli Kupambana..

.

Ila..

.

 Ikifika tu kwenye Tarehe 16 hadi 20 ..

.

Wana *FYEKA* Kamisheni..

.

Wanakubakishia Kidogo..

.

Au ..Wakati wengine 

.

Wana Kuwekea hadi DENI kwenye Kamisheni..

.

NA..

.

Hapo jambo la wewe Kufahamu..ni

.

Kwamba ..

.

Sio wewe Tu Unaekatwa ..

.

Ila mawakala wengi kilio ni hicho hocho.. 

.

NA..

.

Ukweli Hata mimi Walikuwaga Wananikata..

.

Tena mara Mbili  Kila mwezi ..

.

Kwenye tarehe 16 hivi walikuwa wana FYEKA 150k na visenti nabaki na 90k..

.

Ikifika tena Siku moja kabla ya kulipwa Kamisheni..


.

Wanani FYEKA tena kama 80k  nyingine   ..

.

Babaki na 75k hivi 

.

Kutoka kwenye Kamisheni yote  ya 300k na visenti ..

.

Nalikuwa naambulia 75k..tu

.

SO..

.

Nafahamu vizuri ni jinsi gani ..

.

Inavyo umaga kukatwa Kamisheni..

.

ISIPOKUWA TU..

.

Mimi Niliwaza Tofauti Kidogo..

.

Na ...

.

kuchukua Hatua Sitahiki Mimi kama mimi..

.

Wala Hata sikuwapigia voda simu Kulalamika ..

.

Au kuwauliza tatizo ni nini haswa..

.

Nisikilize Vizuri hapa..

.

Iko hivi..

.

..Sio kwa sababu kwamba labda nilifanya Makosa..

.

 Wao  wanaiita FRAUD ..

.

HAPANA...

.

ILA..Kwasababu..

.

Taratibu zao wenyewe Zina Ku- FORCE ufanye makosa ..

.

Hata Kama hupendi..

.

Mfano tu..

.

Watakwambia Usimtumie ..

Mteja aliye Mbali..

.

Swali la Kujiuliza wameshindwa Kuweka..

.

 Mfumo Una Zuia Mhamala wa Aliye Mbali ?..

.

Ila ..

.

watauruhusu mhamala uende tu ..

.

Ili wakuhesabie kosa badae wakukate Kamisheni..

.

POINT nikwamba ..

.

Tusiwalaumu kwa chochote..kwa sababu 

.

Lawama zetu Hazitobadilisha chochote..

.

ILA..

.

Tunapaswa Kufanya yafuatayo..ili kuepuka Kukatwa.. Kamisheni ..

.

NA ..

.

Toka Niaze Kufanya Haya..

.

VODA hawajarudia tena Kunikata kamishenii hata Senti.. 

.

NA..

 .

Ni Vizuri Kwanza Ujue Nini haswa Kinafanya mpaka  ukatwe.

.

Na jinsi gani Ufanye sasa..

.

Na haya ndo ..

.

MAKOSA 6 yanayofanya Ukatwe Kamisheni na 

.

Jinsi gani ya Kuyaepuka..

.


1️⃣Unavunja Mihamala ya LIPA- 

.

..Una Pokea 600k kwenye lipa yako ..

.

Unaigawa mara 2 au Zaidi Kwenye Lipa Zingine ..Kisha unajitolea Kwenye Till ako ili upate Kamisheni zaidi..

.

Hapo unajimaliza..kwasababu VODA..

 .

Wana Mfumo wa Kujua chanzo na mzunguuko wote wa Flot inayoingia kwenye till ako..


.

Hivyo EPUKA kuvunja Mihamala ya LIPA 


Badala Yake fanya Hivi..

.

Ukikusanya  800k au zaidi  kwenye lipa ako

.

 Itoe yote mara moja BILA kuigawa kwa kuhamishia lipa nyingine..

.

Kama una lipa zaidi ya moja..

.

Hakikisha kila kila inapokea malipo moja kwa moja kutoka kwa Mteja..

.

 sio kutoka kwenye lipa yako nyingine..

.

2️⃣Unahamisha Flot ya VODA Uliyopokea Kwa Wakala kwenda Wakala mwingine..

.

Unaingiziwa  Flot 500k unahudumia Kidogo  wateja wawili au watatu ..kisha 

.

Unatoa tena kwa wakala mwingine ...hata Kama unatoa kwa wakala mkuu ..

Bado ni kosa..

.

Kwa sababu lengo la Kuingiziwa Flot na wakala mkuu..

.

ni Wewe Wakala uitumie kuhudumia wateja ..

.

Na sio wewe kuitumia Kidogo tu kisha uitoe tena kwa wakala wenzako..au mkuu..tena

.

Ni kosa hilo kubwa ..

.

Badala Yake fanya Hivi..

.

Flot Utakayoingiziwa na wakala au wakala mkuu..

.

Hakikisha unaitumia yote kuhudumia wateja..hadi iishe yote..

.

Toa tu kwa wakala mkuu Flot iliyo tokana na wateja tu ..

.

sio Ya Ulingiziwa na wakala au wakala mkuu..


NB.

.

Flot iliyotokana na  LIPA ni sawa na Flot ya Mteja aliyetoa kawaida..

.

Hivyo haina madhara yoyote  kuitoa kwa wakala mkuu ..

Ni salama kabisa..

.


3️⃣EPUKA kabisa Kutolea..

 Kwenye Till ako Flot Ya Lipa

.

 Kutoka kwenye Lipa Yenye Majina Sawa Na Till yako..

.

Kwa sababu Kwa Kanuni Za VODA Wakala Hupaswi Kutumia Lipa ..

.

Hivyo kujitolea kwenye till yako kutoka kwenye Lipa yako yenye usajiri sawa na Till.. yako

.

Ni kosa la wazi wazi kabsa..

.

Badala Yake fanya Hivi..

.

Tolea lipa Zingine ambazo ni Tofauti na TAARIFA zako za till...

.

ila Kumbuka tu kuvunja Mihamala..

.

4️⃣Unamuwekea  mteja Zaidi ya mara moja kwa siku..namba hiyo hiyo..

.

Hili ni kosa kubwa..

Na asikudanganye mtu..

.

Eti mwisho mara tatu kwa siku..  HAPANA..

 .

Ni mimi sikwambii ni mara ngapi kwa siku..

.

Ila ..kama Hutaki kufanyia Kamisheni hewa ..

.

Usirudie  kutuma Mhamala wowote zaidi ya mara moja kwa siku..

.

Mteja akirudi tena..Kuweka kwa namba uliyokwisha weka siku hiyo...

.

Mwelekeze tu. Kisitaarabu kwa wakala mwingine...

.

Acha taamaa au huruma ya hasara  itakuponza..

.

5️⃣Unaweka kwa Wateja walio Mbali ..

.

Na hapa elewa kwamba ..

.

 Tunaposema Mteja aliye mbali ..

.

hatumaanishi Tu Aliye mkoa au wilaya nyingine..tu..

.

Hata aliye mkoa uliko au wilaya anaweza kuwa mbali pia..

.

Kwa sababu..

.

 hapa kigezo kinachotumika ni MINARA..

.

Tambua kila eneo lina mnara wake ..

.

Hivyo Wakala Ukituma pesa kwa mteja aliye Na eneo la MNARA uliko mda huo..

.

Basi huyo pia ni mteja aliye mbali..

.

Kwa kwa Kanuni za voda..

.

Hilo ni kosa kabsa..

.

Kwa sababu..

.

Kanuni Zinakutaka wakala 

Umwekea mteja..aliyepo

.

 hapo hapo eneo lako la kazi..

.

Na hapa naomba uelewa kwa nini Wameweka kanuni hii..

.

#1 Ukimuwekea mteja aliye mbali Unawakosesha hela ..

.

Kwa sababu..aliye mbali wanataka atumiwe na mteja mwenyewe kwenye simu simu ake.

.

Ili wamkate mteja kwanza uliyemwekea anavyotuma..

.

Kisha na kule anakotuma wakate anavyotoa au kutuma tena..

.

Hivyo Kanuni hii Ni FAIDA kwa mtandao..

.

Hivyo unavyoivunja kanuni hii ni Kosa  ..Unawakosesha FAIDA..

.

Na Wataichukua pesa yao kwa kukukata Kamisheni..yako


.

#2 Ukimuwekea mteja aliye mbali Sio Salama kwako wakala (Ni Risky)..

.

Ndo zile kesi ..mara mteja anarudi kwako anakwambia haijafka..

.

Bahati mbaya..umefuta na ujumbe..

.

Vi vile tu wengi hatujui ..ila 

Mambo ya fedha hayahitaji ushikaji wala  kuchukulia poa..

.

 Ndio maana mawakala tunakubwa sana  na vikesi vingi ofsni kwa sababu ya ...

.

Taamaa ya kutaka kujipatia FAIDA tu na kupuuza ..

.

Kanuni na Taratibu..

.

Badala Yake fanya Hivi..

.

Mwambie kabsa mteja bila kupepesa macho. ..

.

Kwamba Unapaswa Kumuwekea kwenye namba ake..

.

kisha yeye atamtumia mtu anayetaka kumtumia..


LAKINI..

.

Niwe tu mkweli Kanuni hii 

Ni ngumu..Kuifuta..

.

Na sio Mara zote VODA..

Kukata Kamisheni..

Kwa sababu hii..

.

Ila ..

.

Wakiamua Wanakata..

.

Kwa sababu wewe Mwenye ni shahidi..

.

Kuna kipindi walikuwa hawakukati Kamisheni ..

.

na ulikuwa unatuma kwa mteja yeyote hata aliye mbali..

.


Sasa DAWA yake ni nini haswa?..


.

Ni wewe kuchagua Ufuate..Kanuni 

.

ILI..

.

utakachokipata hata Kama ni kidogo ukipate chochote..

.

Au ufanye unavyopenda..

ILA..

.

VODA wakikata Kamisheni yako..Uwe mpole..

Usilalamike...


Huu ndo Ushauri wangu kwako wakala..


Na..


Usichoke Kujifunza..

Hivyo..

Endelea Kugundua SIRI..

Nyingine  Kuhusu  Uwakala Kwa ..


Kufungua Posts Zingine Zinazofuata..


Chini baada ya Hii..

Mimi Ushauri wangu kwako ni huo..

Thursday, June 20, 2024


 Ufanyeje MAMA AKO atoe Hela BURE kwa Kwa Wakala?

.

Ni hivi....

.

Ili mzazi ako atoe hela BURE kwa Wakala ...


Unapomtumia ..Fanya Hivi. ..


Kwanza ..LAZIMA wewe Umtumie moja kwa moja Kutoka Kwenye Line yako ..


Ya kawaida kati ya mitandao hii..

 .

Kutoka voda ako .

.

Au

Kutoka Airtel ako ..

.

Au 

Halotel Ako..



KUTOKA VODA AKO..


Fanya Hivi..

.

Piga *150*00#


1.Kutuma Pesa 


1.Weka namba ya simu

.

Ingiza Namba Ya mzazi wako (Airtel, Tigo, au Halo)

.

Ingiza KIASI mfano 15,000

.

Ingiza namba yako ya siri


.

Thibitisha kwa Kubonyeza 1


 *ZINGATIA* 

.

Usiende Kutuma Kwenda Mitandao mingine -HAPANA

 

ILA..


Nenda moja kwa moja

.

 Kwenye weka weka namba ya simu..

.

Tazama Mfano wake rahisi 

Kwa..

Kugusa Video hii mara Mbili 

πŸ‘‡



Endelea Kugundua Zaidi 

Kutuma Kutoka Kwenye Airtel na Halo yako

Kwa ..


Kufungua POSTS zinazofuata Chini kabsa

..








Endelea Kugundua Zaidi ..

.

Kutoka kwenye  Airtel ako na halopesa ako..

.

Kwa kufungua Post Zinazofuata Chini kabisa Shuka..

Friday, June 14, 2024


 ONA BURE KUTOA PESA ILIYOTUMWA 

KWA MESSAGE (AIRTEL MONEY)


Fanya Hivi Kutoa pesa iliyotumwa kwa Message ..

.

(WAKALA WA AIRTEL MONEY)..

.

Ndani Ya SEKUNDE 60 

.

Naenda kukuonesha Jinsi Ya Kufanya..

.

ILA..

.

Kabla Sijasahau..

.

Hakikisha Umesha jiunga BURE ..

.

NA..

 GRUPU LA Mawakala Wote Wa Huduma Za Kifedha Tanzania 

.

Inaitwa "WAKALA CLINIC "

.

GUSA Hapa Kujiunga Bure ..

πŸ‘‡πŸ‘‡

[https://chat.whatsapp.com/GcTnu83x7SZFJzVkvvGonH]

.

Kama TAYARI Tuendelee..

.

Wakala wa AIRTEL MONEY 

.

Piga MENU kama Kawaida ..

πŸ‘‡

 *150*60#


2.Toa Pesa


.

1.Toa Pesa Kwa Meseji

.

Ingiza kiasi cha pesa

.

(Kilichotumwa Kwenye Message ya Mteja)

.

Ingiza namba ya simu ya Mteja Iliyo pokea pesa

.

MFANO..

.

Mteja aliyepokea kwa Mpesa 

(0757967955)

.

Halotel (06257967954)

.

KISHA..

.

Ingiza namba ya siri ya kutolea  iliyoko kwenye Message ya Mteja

.

Wakala weka namba yako ya siri ya AIRTEL money ..

.

ILI..

.

Kuthibitisha Mhamala uje Kwako ..

.

NA..

.

Hapo tayari Pesa Iliyotumwa kwa Message 

.

Itaingia Kwako ..kama ilivyo

.

Na utapata commission 

.

Mda huo huo..

.

TAZAMA..

.

Jinsi inavyokuwa Kwenye 

.

Video Hii FUPI..

πŸ‘‡



.

NA..

.

ENDELEA...

.

Kugundua Zaidi..SIRI za 

.

Uwakala kwa Kupitia

.

Posts Zingine zilizoko 

.

Chini

πŸ‘‡


Thursday, June 13, 2024

POSHO SABA( 7) ZA WAKALA


 Ziko njia 7 kwenye uwakala 

Ukizitumia Leo Zitakuingizia Elfu 20k + Ya ziada kila Siku


.

Njia hizi saba ni Tofauti kabisa na LIPA au kuuza vifurushi..

.

7️⃣Charge sh.500 Kutoa Kwa Message

.

6️⃣Kutoa  Kawaida Mteja Mwenye Lipa namba Charge sh.500

.

5️⃣Malipo yote ya serikali (Kuntrol namba) Fanyia sh

500

.

 4️⃣Uza Vocha ndogo 600sh Kubwa 1200sh


NB ..

.

Usipokee.. kumwekea mteja chini ya elfu5(Hutouza vocha zako Wataweka kwenye simu zao)

.

3️⃣ Uza umeme kwa sh.200/=

.

2️⃣Fanyia 1000sh kutuma Flot ya Lipa Voda Kwa mteja anayetaka Flot ya Lipa voda.

.

1️⃣ Fanyia sh 1000 Kumpa Flot au cash wakala mwenzako..


NB:

Kumbuka Lengo lako wakala sio Kukaa Ofsini na

.

 kuhenyeka au kuwa busy tu

.

Lengo  ni Kuingiza FAIDA Usogee mbele Kimaisha..

.

Kama umenielewa Mungu akubariki..

.

Nakutakia Mafanikio kwenye kazi yako ya uwakala!

.

KUMBUKA  KU-SHARE BURE 

.

Kwa wengine 

.

UMEPEWA BURE 

.

Sehemu Ya wewe Kushare BURE 

.

Ni Hapo Chini Sehemu Ya 

.

FACEBOOK..


πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Wednesday, June 12, 2024

Gundua Hapa SHORTCUT ya Kuwapata Kirahisi Watoa Huduma wa VODA kupitia Namba 100

 Hii Ndo SHORTCUT ya Kuwapata Kirahisi..

.

 Watoa Huduma wa VODA kupitia Namba 100

.

Kwenye namba yako ya voda ya kawaida ambayo sio ya uwakala ..


.

Lakini kabla ya yote..

Kama bado hujajiunga ..


Na grupu la ..

.

"WAKALA CLINIC "

..

Omba kujiunga Bure..

.

Kwa kugusa hii link 

Hapa 

πŸ‘‡πŸ‘‡

[https://chat.whatsapp.com/GcTnu83x7SZFJzVkvvGonH]

.


Sasa tuendelee ..


Anza hivi..

.

πŸ‘‰piga 100 -karibu vodacom huduma kwa wateja .

.


πŸ‘‰ Bonyeza 0 kuendelea

.

πŸ‘‰Bonya1 huduma za mpesa

.

πŸ‘‰bonyeza 1 kama umesahau namba yako ya siri

.


 *ZINGATIA* ..

.

voda waliondoa ile ya kusema "kuongea na Mtoa huduma bonyeza namba flani".

.

Ndio maana inabidi ujifanye

.

 kama umesahau namba ya siri 

.

hapo ndo utawapata ..


.

Bila hivyo utakesha unabonyeza bonyeza simu

.

 bila kuwapata..

.

Endelea na mchakato..

.

πŸ‘‰bonyeza 2 Kupata msaada kwa wahudumu kufunguliwa account ya mpesa ..

.

πŸ‘‰1 kwa tatizo la namba ya siri 

.

πŸ‘‰1 namba imesajiriwa kwa majina yako..

.

πŸ‘‰2 hajatoa pesa ndani ya siku saba..

.

Hapo mtoa huduma kwa wateja atapokea ..

.

Wewe utamweleza shida zako..

.

Hata Kama sio ya namba ya siri ..

.


Bila hivyo huwezi kuwapata

.


 Ahsante kama umenielewa 

🀝


NA..

.

Kama kuna jambo lolote linakutatiza kuhusu Mitandao ya simu..

.

Niandikie tu hapo chini kabisa..

.

Sehemu Ya comments..

.

Ili nikupe majibu yake Leo Leo kwenye post inayofuata..


.

PIA..

.

Endea Kugundua na..

 Kujifunza Zaidi SIRI nyingine ..

.

Kuhusu Mitandao ya Simu..

.

Kwa Kuangalia post nyingine..

.

Zinazo fuata chini

πŸ‘‡πŸ‘‡

Wakala Fanya Hivi Iwe Ina Leta Jina Lako Kwanza  Kabla Mteja Wa Airtel Hajathibitisha Anapolipa  Kuja  Lipa Voda Ako

 Fanya Hivi Ileta JINA 

.

Mteja wa Airtel Anapolipa Kuja VODA ..

.

Mteja(Airtel ) apige..

.

*150*60#

.

1.Tuma pesa

.

2.Tuma mitandao mingine

.

2.M-PESA

.

2.Weka Lipa Namba ya M-PESA 

.

1.Weka Lipa Namba Ya M-pesa

.


(Aingize Lipa Yako ya VODA)

.

Aingize kiasi

.

Italeta JINA lako Kabla

.

 Hajathibitisha kwa namba ya siri


.

Ahsante kama umepata kitu

.

PIA..


Ikiwa una jambo lolote..

.

Kuhusa uwakala na Lipa..

.

Linalokutatiza..


Niandikie tu Sasahivi..


Hapa chini ..sehemu Ya comments..


Nami ntaitolea majibu Leo Leo..


Kwenye post inayofuata..

.

PIA..


Endea Kugundua na Kujifunza ..

.

SIRI nyingine Za Uwakala 


Kwa Kutazama na Ku-SHARE 


Post Zingine Zinazofuata


Chini ..

πŸ‘‡

Tuesday, June 4, 2024

Karibu Wakala clinic blog

 Karibu sana kwenye blog ya Wakala Clinic  ya kwanza Tanzania Kwa kutoa elimu Bora 

Ukiwa na tangazo lolote leta utangaziwe kwenye blog hii Kwa Bei ndogo tu

Wasiliana nasi Kwa WhatsApp   +255757967954

karibu sana