Matokeo FORM SIX 111056 Wapasua.
#HABARI Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita (Form Six) ambao ulifanyika mwezi wa tano mwaka huu ambapo katika tathmini ya jumla ya matokeo hayo imeonesha jumla ya watahiniwa 111,056 wa Shule za kujitegemea sawa na 99.43% ya Watahiniwa wenye matokeo ya mtihani huo wamefaulu.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania NECTA, Dr. Said Mohamed, amesema katika matokeo hayo “Wanawake waliofaulu ni 49,837 sawa na 99.61%, Wanaume waliofaulu ni 61,219 sawa na 99.28%, mwaka 2023 Watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 104,549 sawa na 99.23%, hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa 0.20% ikilinganishwa na mwaka 2023”
“Idadi ya Watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 7,804 sawa na 93.34%, mwaka 2023 Watahiniwa wa kujitegemea 8,539 sawa na 92.30% walifaulu mtihani huo, hivyo ufaulu wa Watahiniwa wa kujitegemea umeongezeka kwa 1.04% ikilinganishwa na mwaka 2023”
#Wakala Clinic
0 comments: