Saturday, September 14, 2024

Jinsi Wakala Mdada Alivyo Taperiwa Sh.800,000


 **Jinsi Wakala Mdada Alivyo Taperiwa Sh.800,000/=* 


Nimeichukua sehemu..

Nikaona kuna mtu inaweza kumsaidi..


Ni hivii...


Miaka Kadhaa iliyopita kuna dada mmoja alitapeliwa hela 800,000 (laki nane).


Mkasa wake ulikua hivi.


Ofisi yake ipo  karibu na seheme ya kutengezea magari (gereji), 

.

kuna mteja alikuwa anaenda pale Ofisini kutoa hela, huwa anatoa hela nyingi tu 100,000 kwenda mbele.


Anampa simu yule mdada atoe hela then anamuambia chukua 5,000 kunywa soda,


 akawa na muendelezo huo huo anatoa hela anamuachia 10,000 kunywa soda (sasa sijui soda gani inauzwa 10,000 wanawake wenyewe mnajua (Jokes 😂).


Akitoa hela anaenda pale gereji, mwishowe akajitambulisha kwa yule mdada kuwa yeye ni miungoni mwa watu wa pale gereji.


Kuna siku akaja na simu akamuambia angalia salio dada na . ...


namba ya siri anaijua ya mteja wake wa thamani, baada ya kuweka namba ya siri akaona kuna zaidi ya Milioni moja, akamuambia toa 800,000.


Wakati yupo kwenye process za kutoa hela simu ikaita, ikabidi arudishe kwa mteja simu yako inaita.


Mteja akapokea na kumuuliza yule mtu upo hapo gereji ? Basi natoa hapa kwa wakala dakika moja nakuletea.


Baada ya hapo akakata simu akamuambia nipe  800,000 endelea kutoa hapo mimi nampelekea jamaa halafu nakuja kuchukua simu, dada alimuamini sana yule mteja akampa.


Akashika simu aendelee kutoa kila akitoa anaambiwa namba ya siri sio sahihi, 


akaanza kupagawa akaenda gereji hakuna mtu, akauliza kwa watu wa pale wakasema hawamjui.


Basi dada akauziwa kitochi kwa 800,000.


Funzo kwa wadada mlio amua kufanyakazi ya kuchezea hela asubuhi hadi jioni kuweni makini sana


 usione mtu anakuachia vi 2,000,na  5,000 unywe soda ukajua labda anakutaka anashindwa kukuambia, NO,


 wengine wanatumia hizo mbinu hizo kwa manufaa ya kupata zaidi ya hiyo anayokupa baadae.


Natumaini kuna mtu itamsaidia 


Wakala yule yule unayemfahamu 


MR.BROWN

0 comments: